: Solomon Mkubwa – Lipo Jibu [+ Lyrics]


Lipo Jibu Mp3 by Solomon Mkubwa Ft. Upendo Nkone

A soul-lifting song from the African Christian/Gospel worshipper, minister, and song writer “Solomon Mkubwa“, as He calls this song “Lipo Jibu” featuring Upendo Nkone . This song is sure to bless your heart and uplift your spirit.

Get Audio Mp3, Stream, Share, and be blessed.

Lyrics: Lipo Jibu by Solomon Mkubwa

[Verse:1 Solomon]
Unayopitia, limeumiza moyo wako
Unayopitia, imesababisha shinda maishani
Unayopitia, watu hawakuelewi- lakini sio mwisho wa maisha bado kuna jibu
Unayopitia, imesababisha ata pressure zimepanda
Unayopitia, imeumiza akili
Unayopitia, imesababisha watu wakukatae, lakini sio mwsho wa maisha bado kuna jibu

[Upendo nkone)
Nakuona unalia, moyo wako unaumia
Nakuona unalia , maumivu yamepita kipimo
Mawazo yameujaza moyo, wala hujui la kufanya wewe
Ninakushauri tulia, jibu lako linakujaUmejaribu kuomba ushauri, bado hujapata jibu kamili
Umeangaika kwa waganga, bado wewe hujapata suluhisho
Akili zako zimefika mwisho, wala hujui hufanye nini
Nina kushauri tulia, jibu lako linakuja

[Chorus]
[ Lipo jibu × 3] Mwachie bwana
[ Lipo jibu × 3] Bwana atatenda
( Repeat)

[ Verse: 2 Solomon ]
Mengine majaribu yanayotupata
Ni shule mbele zetu
Kubali shule ya mungu, kusudi ufaulu maishani
Haujui ya kesho, Mungu anayajua
Sio mwisho wa maisha, jikabidhi kwa bwana
Mengine ni majaribu tu, na yanatufunza kiimani
Yanatufanya tusimame ili wengine tuwape shauri
Watakayo yapitia, wakija kwetu tuwahimize moyo
Mungu ni mwaminifu, anajua unakoenda

[Upendo]
Usidhani kujinyonga kwako, ndio suluhisho la matatizo
Usidhani kuuondoa uhai, ndio utakuwa umeyakomesha
Huo ni uongo tu wa adui, anataka kukuharibia wewe
Usijidhuru kwa lolote, wewe mungojee bwana
Ayubu alijaribiwa,
Mali zake zote zikaisha
Watoto wake nao wakafa
Aliyapitia mambo mazito
Lakini Ayubu alivumilia, alayashinda majaribu yoote
Na wewe ndugu yangu jipe moyo, ushindi wako unakuja

[Chorus]
[ Lipo jibu × 3] Mwachie bwana
[ Lipo jibu × 3] Bwana atatenda
( Repeat)
(Speaking)
Usifadhaike..
Macho yake yanaona
Yanaona watu wote duniani
Tena anawapenda wote wenye mwili
Eeeeeeeeeeee
Skia, inawezekana kabisa umefikia mwisho. Mwisho wa akili yako
Lakini kumbuka kwamba yesu anaweza kukuinua tena
Yesu anaweza kukuponya tena
Maana yeye anaweza mambo yote
Usijali, usivunjike moyo atafanya kwa ajili ya jina lake
Hallelujah